Advertisement

Temeke wapewa vifaa kujikinga na corona, Meya atoa neno

Wednesday April 15 2020
pic temeke

Dar es Salaam. Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Abdallah Chaurembo  amewataka  wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na  ugonjwa wa corona.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 15, 2020 wakati akipokea vitakasa mikono, barakoa na glovu kutoka kampuni  ya General Petroleum.

Chaurembo amesema wananchi wafuate maelekezo ya wataalamu kwa kuwa Temeke ni moja ya manispaa zenye wagonjwa wa corona.

"Msaada huu umekuja wakati muafaka kwa ajili ya wananchi wa Manispaa ya Temeke. Vifaa hivi vimesambazwa kwenye hospitali ya rufaa ya Temeke na hospitali ya Wilaya ya Mbagala Zakiem pamoja na kata zote 23 za manispaa, pia tuendelee kuchukua tahadhali kama  Serikali inavyotutaka,” amesema  Chaurembo.

 

 

Advertisement

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo amesema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa ugonjwa huo hauna tiba na wachukue tahadhari kwa kuepuka msongamano na kushikana kwa mikono.

Ofisa rasilimali watu wa kampuni hiyo, Aboubakar Kondo amesema wametoa msaada wa barakoa 1200, glovu 1200 na vitakasa mikono 1000.

Kondo amesema kampuni hiyo imeunga mkono Serikali kupambana na maambukizi ya corona na hawataishia Temeke watafanya hivyo katika wilaya za Ilala Kinondoni na Ubungo.

 

Advertisement