Vibonzo vya kumkosoa rais marufuku Rwanda

Friday April 26 2019

 

Kigali, Rwanda. Mahakama Kuu Rwanda imetupilia mbali madai yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya wanasheria nchini humo kupinga sheria iliyoanzishwa mwaka jana kuwa ni kosa la jinai kuchora vibonzo vinavyomkejeli Rais wa nchi hiyo.

Mahakama Kuu nchini Rwanda imetupilia mbali madai yaliyotolewa na baadhi ya wanasheria nchini humo kupinga sheria iliyoanzishwa mwaka jana kuwa ni kosa la jinai kuchora vibonzo vinavyomkejeli Rais wa nchi hiyo.

Wakati huohuo wanasheria wamefungua kesi kulipinga hilo huku wakisema masharti hayo ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Hata hivyo mahakama hiyo imeamua kuwa viongozi wengine waandamizi serikalini na viongozi wakuu wa kidini halitakuwa kosa la jinai kuwachora kwenye vibonzo.

Akizungumza na DW, mkuu wa jopo la mawakili waliokuwa wameishitaki Serikali kuhusu sheria hiyo Richard Mugisha, amesema wao kama wanasheria wameridhika na uamuzi wa kuondolewa baadhi ya vipengele kwenye sheria hiyo.

Advertisement