Waioshio na VVU waomba kutibiwa bure magonjwa sugu

Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wilaya ya Kilombero wameiomba Serikali kupitia wizara ya afya kuwapa msamaha wa gharama za huduma za matibabu ya magonjwa sugu yanayoambatana na VVU.

BY Hamida Shariff, Mwananchi. hshariff@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za Kulevya ilitembelea vikundi vya watu wanaoishi na VVU, Morogoro.

Advertisement

Kilombero. Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wilaya ya Kilombero wameiomba Serikali kupitia wizara ya afya kuwapa msamaha wa gharama za huduma za matibabu ya magonjwa sugu yanayoambatana na VVU.

Ombi hilo limewasilisha hivi karibuni kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Dawa ya kulevya ilipotembelea kikundi cha wajasiriamali cha Upendo ambacho kinaundwa na watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

Mwenyekiti wa Baraza la watu wanaoishi na Vvu wilayani humo (Konga) Hilda Kumba ameyataja magonjwa hayo sugu yanayowasumbua kuwa ni Sukari, Shinikizo la damu, figo na Kifua Kikuu.

Hilda amesema bado serikali haijatoa msamaha wa gharama za matibabu kwa watu wanaoishi na VVU hivyo wenye kipato kidgo wanashindwa kumudu gharama hizo na hivyo wengi wao hufariki dunia.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kikundi cha watu wanaoishi na Vvu cha Upendo Merisia Yengulla aliishukuru Halmashauri hiyo kwa kutoa ruzuku ya Sh1 milioni kwa kikundi hicho ambacho kwa sasa kimepata faida ya Sh 11 milioni kutokana na shughuli za ushonaji mikeka, kilimo na ufugaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya bunge, Oscar Mkasa ameipongeza halmashauri hiyo kwa kusimamia kikamilifu ruzuku wanayotoa kwa vikundi hivyo vya watu wanaoishi na VVU.

More From Mwananchi
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept