Walichokisema ndugu kuhusu ajali ya Mkuranga iliyosababisha vifo 21

Wednesday April 15 2020

Ni simanzi. Ndivyo unavyoweza kusema ukizungumzia ajali iliyotokea leo asubuhi Jumanne Aprili 15, 2020 katika kijiji cha Magawa kilichopo wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani na kusababisha vifo vya watu 21 na majeruhi 17.

Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga amesema watu 18 walifariki katika ajali hiyo na wengine 15 kujeruhiwa lakini baadaye taarifa  za hospitali ilieleza kuwa watu 17 waliofikishwa wakiwa majeruhi, watatu waliaga dunia.

Mwananchi lilifika eneo la tukio na katika kijiji cha Magawa na kuzungumza na watu walioeleza kwa hisia vifo vya ndugu zao akiwemo mmoja aliyedai ndugu yake alikuwa anafunga ndoa Jumapili Aprili 19, 2020.

Advertisement