Wamiliki kiwanda cha Nyuzi walalamikia ukosefu wa masoko

Wednesday October 2 2019

Waziri wa Viwanda na Biashara,Innocent

Waziri wa Viwanda na Biashara,Innocent Bashungwa,akiangalia vitambaa vinavyoyengenezwa na kiwanda cha New Tabora textile kwa ajili ya kufungia marobota ya pamba.picha na Robert Kakwesi 

By Robert Kakwesi,mwananchi.co.tz

Tabora. Wamiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Mjini Tabora, New Tabora textile, wamelalamikia ukosefu wa masoko ya Nyuzi jambo linalowafanya wasifanye kazi kwa tija.

Akitoa taarifa kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, katibu wa kiwanda hicho,Jotam Paschal, amesema masoko yamekuwa shida kwao na wanahangaika kupata Biashara ya kuuza Nyuzi zake.

Ameiomba Serikali isaidie kuwatafutia masoko ili waweze kuendelea na uzalishaji kwa tija kwani hata gharama za uzalishaji amedai ni kubwa.

Ametoa mfano wa umeme kuwa kama mashine zinafanya kazi kwa wingi wake,gharama zinafikia Sh50milioni,akisema ni kubwa.

Akieleza changamoto wanazokumbana nazo, amesema wanashindwa kupata pamba iliyochambuliwa na ukosefu wa kinu cha kuchambua pamba.

Advertisement