Wanaharakati wa CPJ waliokamatwa waachiwa ‘huru’

Muktasari:

Wanaharakati wa Kamati Maalumu ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) waliokuwa wamekamatwa wameachiwa huru huku hati zao za kusafiria zikiendelea kushikiliwa

Dar es salaam. Wanaharakati wa Kamati Maalumu ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) wameachiwa 'huru' lakini duru za habari zinasema hati zao za kusafiria zinashikiliwa.

Wanaharakati hao Angela Quintal na Muthoki Mumo walioingia nchini Tanzania mwanzoni mwa wiki hii walikamatwa na maofisa wa Serikali jana usiku Jumatano wakiwa katika hoteli ya Southern Sun. Hata hivyo habari ambazo Mwananchi imezipata ni kwamba waliachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa.

Hata hivyo, hadi saa 5 asubuhi hati zao zilikuwa zimeshikiliwa hali inayowafanya waendelee kuwa njia panda na wao wakiwa wamerejeshwa katika Hoteli ya Southern Sun

Awali, leo  asubuhi Alhamisi Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania ilisema inafuatilia taarifa zilizosambaa zinazodai kwamba vyombo vya dola kwa kushirikiana na idara hiyo vinawashikilia wanaharakati hao.

Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda alisema, "Na sisi tumeziona hizo taarifa mtandaoni ila hatuna taarifa ya kukamatwa hao wanaharakati na idara yetu.”

Endelea kufuatilia Mwananchi