Advertisement

VIDEO: Wazee wamkaribisha Maalim Seif kuwania uraisi kupitia Chadema

Wazee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kipo tayari kumkaribisha Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kuwania urais kupitia chama hicho.

Mwenyekiti wa Baraza la wazee Chadema ,Hashim Jumaa Issa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya kisiasa nchini.Picha na Said Khamis 

BY Hussein Issa, Mwananchi hissa@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

  • Ni baraza la wazee la Chadema ambao wamemshauri Maalim Seif Sharif kuhamia Chadema na kuwania urais kupitia chama hicho.

Advertisement

Dar es Salaam. Wazee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kipo tayari kumkaribisha Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kuwania urais kupitia chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 11 Mwenyekiti wa Wazee wa Chadema, Hashimu Juma amesema kutokana na mgogoro unaoendelea CUF,wameona kuna kila sababu ya Maalim Seif kuhamia Chadema.

Wazee hao wamesema wameshafanya naye (Maalim)mazungumzo ya awali.

Pamoja na mambo mengine wamesema hakuna sababu ya kufanyika chaguzi za mara kwa mara kutokana na kujiuzulu kwa viongozi hasa wabunge na madiwani.

Mwenyekiti huyo wa Taifa amesema gharama za chaguzi hizo zinatokana na kodi za wananchi.

More From Mwananchi
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept