Waziri Bashungwa akerwa na utendaji wa kiwanda cha Nyuzi Tabora

Wednesday October 2 2019

Waziri wa Viwanda na Biashara,Innocent

Waziri wa Viwanda na Biashara,Innocent Bashungwa,akiangalia vitambaa vinavyoyengenezwa na kiwanda cha New Tabora textile kwa ajili ya kufungia marobota ya pamba.picha na Robert Kakwesi 

By Robert Kakwesi,mwananchi [email protected]

Tabora.Waziri wa Biashara na Viwanda,Innocent Bashungwa,ameonesha kukerwa na kutofanya kazi kikamilifu, kiwanda cha Nyuzi Tabora na hivyo kutofikia lengo la Serikali la kutaka kuwa na uzalishaji mkubwa wa Nyuzi na kuongeza ajira.

Akizungumza baada ya kukagua shughuli zinazofanyika kiwandani hapo,Waziri huyo, amesema hajaridhika na utendaji kazi wa kiwanda hicho na malengo ya Serikali hayajafikiwa.

"Ubinafsishaji ulikuwa na nia njema na bahati mbaya hapa nimekuta ubabaishaji" Amesema

Amesema inaelekea waliochukua kiwanda hicho,hawqkuwa wamejiandaa na kisema wazi kuwa hajaridhika na utendaji kazi wa kiwanda hicho.

Amesema Serikali itaangalia namna kitakavyoweza kuzalisha kwa tija na kukitaka kiwe tayari kubadilika kwa lengo la kutimiza azma ya kubinafsishwa kwake.

Katibu tawala wa Mkoa wa Tabora, Msalika Makungu,amesema wamiliki hata taarifa zake hazipo wazi na hivyo kuwa vigumu kuona namna ya kisaidia.

Advertisement

Amesema kiwanda hakina mpango wa Biashara tangu awali na kuwa vigumu kujua mpango gani unawaongoza katika utendaji wake wa kazi.

Advertisement