Wema Sepetu afikishwa mahakamani Dar

Muktasari:

Mwigizaji  na mlimbwende  wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo saa 4 asubuhi

Dar es Salaam.  Mwigizaji  na mlimbwende  wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018.

Wema amefikishwa mahakamani hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa katika chumba cha mahabusu.

Amefikishwa mahakamani hapo akisindikizwa na polisi huku akiwa amevaa miwani na kujitanda ushungi.

Jana, zilisambaa taarifa kuwa Wema alikuwa akishikiliwa na polisi, taarifa ambazo si polisi wala watu wa karibu wa mwigizaji huyo waliokubali kuzithibitisha.

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa taarifa zaidi