Zitto: Kupigwa risasi Lissu unahitajika uchunguzi wa kimataifa
Muktasari:
Amesema kwamba washambuliaji wamelenga kuwanyamazisha
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema unahitajika uchunguzi wa kimataifa dhidi ya shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Akituma ujumbe wake kwenye Twitter, Zitto amesema kwamba vyombo vya ndani vinaweza visiaminike kutokana na uzito wa tukio hilo.
Amesema kwamba ‘’Washambuliaji wa Lissu wamelenga kutunyamazisha. Iwapo tutaendelea kunyamaza, watashinda. Hatuwezi kuwapa nafasi hiyo, tunaongea kuhusu haki,”amesema.
Lissu alishambuliwa Alhamisi wiki hii wakati alipokuwa akifika nyumbani kwake mjini Dodoma akitokea katika vikao vya Bunge.