Zitto ahofia kufutwa kwa NGO, adai kuna walengwa

Monday June 24 2019

 

By Kelvin Matandiko Mwananchi [email protected]

Dar es salaam. Kiongozi wa Chama cha upinzani nchini Tanzania cha  ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Bunge wanataka kupitisha mabadiliko ya sheria kadhaa yanayotishia uhai wa taasisi mbalimbali nchini.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Juni 24, 2019 Jijini Dar es Salaam, Zitto amesema kati ya Alhamisi wiki hii Bunge litawasilisha mswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali, unaohusisha mabadiliko katika sheria ya asai za kiraia (NGOs), Filamu,  Kampuni na Takwimu.

"Kwa mfano mabadiliko ya sheria a Kampuni kifungu cha 400(a) yanaweka tafsiri tofauti kabisa ya Kampuni iliyopo kwa sasa, kwa sasa kampuni ni tofauti na mwenye kampuni, sasa sheria hii inaenda kufanya kampuni na mwenye kampuni kuwa kitu kimoja," amesema.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini amesema, “Kwa hiyo msajili atapewa mamlaka ya kufuta kampuni yeyote, kwa mfano iwapo mwenye kampuni atazuiliwa kuingia nchini Tanzania.”

Amesema endapo mabadiliko hayo yakipitishwa na Bunge kwa hati ya dharura, yataathiri uhai wa NGOs nyingi zikiwamo Taasisi za Benjamini Mkapa, Mwalimu Nyerere, Hakielimu, Twaweza na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC).

Kutokana na mazingira hayo, Zitto amewataka Watanzania nje ya Bunge kupinga mabadiliko hayo, akidai ni kandamizi na yanajenga taasisi kadhaa.

Advertisement

Advertisement