Fahamu namna ajira yako inavyoweza kusitishwa kisheria

Kawaida ni kama sheria. Ni utamaduni wa miaka mingi mtoa huduma kutoa risiti au stakabadhi zenye nembo, jina na rangi ya ofisi yake kwa kila mteja kulingana na huduma au bidhaa aliyonunua. Mara nyingi risiti hizi zimekuwa zikijazwa kwa mkono au kuchapuna wakati uhusiano kati ya muajiri na muajiriwa hufikia ukingoni. Nchini, kuna sheria na utaratibu unaotoa mwongozo wa kuhitimisha uhusiano wa ajira.

Sheria zilizopo ni pamoja na ya ajira na uhusiano kazini ya mwaka 2004, ya asasi za kazi ya mwaka 2004 na ya mikataba.

Kwa mujibu wa sheria, kuna aina nne za usitishaji wa ajira ambao ni ule wa makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriiwa na unaosababishwa na matukio kama kifo au kufa kwa biashara au kazi husika.

Usitishaji mwingine ni kwa mwajiriwa kuamua kuacha kazi na mwajiri kumfukuza au kumwachisha kazi mwajiriwa kwa sababu maalumu.

Ili usitishaji uwe na nguvu kisheria ni lazima uwe halali. Kuhalalisha hili, mwajiri anatakiwa kuthibitisha mambo kadhaa kutoa sababu za msingi kusitisha ajira husika, hakuna uonevu na utaratibu uliotumika umezingatia misingi ya haki.

Miongoni mwa mambo yanayoweza kuhalalisha kuachishwa kazi ni kukosa uaminifu kulikokithiri kama vile kughushi au wizi, kuharibu mali kwa makusudi au kuhatarisha usalama wa wengine. Uzembe uliokithiri, kushambulia na ukaidi uliokithiri ni sababu nyingine.

Vilevile, mwajiri anaweza kusitisha ajira kutokana na mabadiliko ya mahitaji ya uendeshaji wa mwajiri katika usimamizi wa fedha, teknoklojia au kubadili mpangilio wa shughuli kutokana na kuunganisha biashara.

Kabla ya kusitisha ajira za wafanyakazi ni lazima mwajiri ashauriane nao iwe kupitia chama cha wafanyakazi au na wao wenyewe iwapo hakuna chama.

Anapoachishwa kazi, mfanyakazi anastahili kulipwa mshahara kwa kazi aliyofanya kabla ya kuachishwa, kulipwa likizo ambazo hajaenda na siku za likizo ambazo mzunguko wake haujakamilika. Pamoja na hayo, anastahili kulipwa kiinua mgongo, angalau mshahara wa siku saba kwa kila mwaka kamili ambao mfanyakazi ametumikia.