‘Tutaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji’

Saturday November 28 2015Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza. 

By Burhani Yakub

Tanga. Serikali Mkoa wa Tanga, imeahidi kuweka mazingira mazuri zaidi kwa mashirika na wadau wa maendeleo, ili washiriki kuinua uchumi bila kuwapo kwa vikwazo.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza wakati wa uzinduzi wa matumizi ya huduma mtandao ya 4G/LTE mkoani humo inayotolewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdullah Lutavi, Mahiza alisema katika kusukuma maendeleo, Serikali imejipanga kuandaa mazingira yatakayowezesha mashirika na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi wafanye kazi bila bughudha.

Mkuu wa Kitengo cha B2B cha Kampuni ya Tigo, Renee Bascope alisema Tanga ni mkoa wa tatu kuwekewa huduma ya teknolojia ya 4G.

Advertisement