Teknolojia ya mawasiliano ni nguzo muhimu ya ukuaji wa biashara nchini

Muktasari:

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa mbali na kuwa mitandao ya simu hutumika kwa mawasiliano lakini pia mitandao hiyo kwa sasa ni nyenzo muhimu kwa wafanyabiashara wa wadogo (SMEs) katika kukuza uchumi na biashara zao kwa ujumla

Hayo yamo katika repoti iliyotolewa hivi karibuni na taasisi ya GSMA ambapo taarifa hiyo ilisema Sekta hii ambayo inakadiriwa kuwa na wafanyabiashara zaidi milioni tatu nchini kote wanakadiriwa kuchagia zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa (GDP) na kufanya serikali itambue mchango wake hivyo kuiingiza sekta hii kwenye mpango wa taifa wa maendeleo.

Ilisema Mbali na kupiga simu wafanyabiashara hutumia mitandao ya simu kuhifadhi, kutuma na kupokea fedha, kupata huduma bima, kulipia malipo ya vitu na huduma mbalimbali na pia hata huduma kukopa fedha kwa ajili ya miradi au kutatua matatizo yanayowakumba wafanyabiashara wadogo.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa sekta ya mawasiliano ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa SMEs hasa kupitia huduma za vifurushi vya data na sauti ambavyo huwezesha mawasiliano ya kibiashara na hata yale ya kijamii.

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa Kutokana na hali hiyo ni muhimu kuhakikisha sekta hii inaendelea kukua zaidi na zaidi ili wafanyabiashara waendelee kunufaika nayo.

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa msingi wa biashara ni mawasiliano na taarifa kati ya mnunuzi na muuzaji na makampuni ya mawasiliano nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa yanasaidia jumuiya ya wafanyabiashara kukua.

Taarifa hiyo ilitoa mfano kuwa kupitia kampuni ya Tigo katika huduma yake ya Tigo Pesa kwa sasa watumiaji wake wameungwa na mfumo wa malipo wa serikali (Government’s e-Payment Gateway) na kuwasaidia wafanyabiashara Kurahisisha kulipia ankara zao. Vile Tigo Pesa imewasaidia wafanyabiashara kukusanya malipo ya bidhaa zao. Imeonyesha kuwa wateja wa Tigo sasa wanaweza kulipia bidhaa zao kwa kutumia programu ya Tigo Pesa au hata kuwalipa wafanyakazi wao. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa zaidi ya kampuni 70,000 zinatumia huduma za tigo kufanya miamala mbalimbali.

Taarifa hiyo, ilisema ili kuoboresha huduma hii, Tigo imezindua njia ya huduma ya online kwa wateja wake kwa kutumia mtandao wa kijamii ujulikanao kama WhatsApp. Huduma hiyo, inawawezesha wateja kuwasiliana na dawati la huduma kwa wateja moja kwa moja na haraka ili kuweza kurahisisha kutatua matatizo ya wafanyabiashara kwa haraka na wakati wowote.