Airtel Tanzania yazindua huduma ya Tuma na ya Kutolea

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua huduma inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea’.

Huduma hiyo itawawezesha  wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa wapendwa wao, ndugu, marafiki pamoja na wanafamilia bila kukokotoa  gharama ya hela ya Kutolea.

 Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hiyo, mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda alisema uzinduzi wa huduma hiyo ni sehemu ya maadhimisho  wiki ya  huduma kwa wateja ilioanza  Oktoba 7.

“Airtel imedhamiria kuendelea kuhakikisha ya kwamba inatoa huduma bora muda wote na hii ndio sababu tumekuwa tukiwaletea wateja wetu huduma na bidhaa ambazo ni za kiwango cha juu kabisa,’alisema Nchunda.

Aliongeza:  Kwa muda mrefu, tumekuwa tukiona wateja wa Airtel Money wakituma pesa pamoja na ya ziada ambayo lengo lake ni kufidia gharama za Kutolea ambazo ni maarufu kama Tuma na ya Kutolea. Sisi  nia yetu ni kuwapa wateja wetu kilicho bora, leo Airtel imekuja na huduma ambayo ni suluhishi wakati wa kutuma pesa kwani gharama za Kutolea zitakuwa zikikatwa wakati wa kutuma kwa kupitia menu ya Airtel Money.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema, Airtel inatambua kuwa ni muhimu kuweka mahitaji ya wateja wetu mbele.

“Ni kwa kupitia Airtel Money ambapo mteja anaweza kutuma pesa bure na sasa tumekuja na huduma suluhishi kwenye gharama za Kutolea. Tunajivunia kuwa na huduma zenye uwazi ambapo kwa sasa wateja watakuwa na uhakika wa kujua gharama halisi ya kutolea pale wanapotumia huduma ya Tuma na ya Kutolea. Airtel itaendelea kutoa huduma ambazo utapatikanaji wake ni rahisi, nafuu na za haraka ili kukidhi mahitaji ya wateja,” alisema Bi Singano.

Airtel kwa sasa inayo zaidi ya matawi 1,000 Airtel Money  na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 60,000 ambapo wateja  wanaweza kupata huduma zote za Airtel kama vile kusajili kwa alama ya vidole, simu mpya za smartphone, vifaa vya simu pamoja huduma nyingine.

Caption: Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari baada ya kuzindua huduma ya  ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money.