BancABC yazindua akaunti ya IZZE haina makato ya mwezi

Wednesday September 18 2019

 

Dar es Salaam. Benki ya BancABC Tanzania imetangaza kuzindua akaunti mpya ya IZZE ambayo haina makato yeyote ya mwezi.
ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara leo imeendelea kudhihirisha ubunifu wake katika huduma zinazowanufaisha wateja wake baada ya
Kupitia akaunti ya IZZE ya BancABC, mteja anahitaji kuwa na kitambulisho cha taifa tu kilichotolewa na NIDA ili kufungua akaunti hiyo, na atapata riba hata akiwa na kianzio cha Sh10, 000.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua akaunti hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Wateja wadogo na wa kati wa benki BancABC Joyce Malai alisema leo katika soko la biashara watu wengi wanaangalia sehemu watakayonufaika kuwekeza fedha zao na yenye uhakika wa kupata faida manufaa kadhaa.
Malai alisema uhakika wa kupata faida au manufaa ni moja ya malengo muhimu kwa kila mtanzania. Vile vile, kufungua akaunti ya benki kwa siku hizi imekuwa ikichukuliwa kama hatua ngumu yenye kuhitaji muda na zaidi inaonekana kama inalenga watu wenye kipato kikubwa.
“BancABC tumelifanyia kazi suala hilo na ndio sababu tumekuja na akaunti ya IZZE ambayo ni rahisi kufungua kwani mteja anaweza kufungua akaunti hii hata kupitia mawakala wetu popote nchini,” alisema Malai.
Malai aliongeza kuwa akaunti ya IZZE ni Rahisi kufungua kama ilivyo jina lake. Mteja anahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa tu na haina kiasi chochote cha kuanzia, haina makato ya mwezi na muhimu zaidi ni kwamba mteja anapata riba kila mwezi ikiwa ana salio kuanzia Sh10, 000 au zaidi kwenye akaunti yake.
Akaunti hii imeunganishwa kwenye mtandao wetu wa BancABC Mobi kupitia USSD (*150*34#) na Aplikesheni yetu kwa hivyo mteja haitaji kila mara kutembelea matawi yetu kwa ajili ya kuweka au kutoa fedha.
Meneja wa huduma za uwakala wa benki hiyo, Mwita Rhobi alisema BancABC imewawezesha mawakala ambao wanapatikana nchini kote kusaidia ufunguaji wa akaunti ya IZZE.
Mawakala hawa wataweza kufanya hatua zote za kufungua akaunti kidigitali na mtu yeyote anayehitaji kufungua akaunti ya IZZE atafanikisha huduma hiyo kwa muda usiozidi dakika tano na papo hapo mteja anaanza kuweka pesa kwenye akaunti yake kupitia aidha mawakala wetu wa BancABC, matawi yetu ama kupitia kuhamisha fedha kutoka kwenye mitandao ya simu kwenda kwenye akaunti yake aliyoifungua kirahisi kabisa.
 “Natoa rai kwa kila Mtanzania mwenye kitambulisho cha Taifa (NIDA) kutembelea tawi lolote la BancABC au mawakala wetu kufungua akaunti ya IZZE kwa urahisi kabisa na kupata manufaa kedekede kama mlivyosikia hapo awali,” alisema Rhobi.

Advertisement