Dar kuutumia ukuta wa bahari kibiashara

Monday June 11 2018

 

Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam limetoa wiki mbili za kupata ushauri juu ya matumizi sahihi ya ukuta uliojengwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi, ili kuliongezea mapato.

Hilo limebainishwa na meya Isaya Mwita alipozungumza na gazeti hili kuhusu mikakati ya kuutumia ukuta huo wenye urefu wa mita 920 pembezoni mwa Barabara ya Barrack Obama.

Miongoni mwa mipango iliyopo, Mwita alisema ni kuifanya sehemu hiyo iwe forodha kama ile ya Zanzibar ambayo watu hupumzika huku wakipata huduma mbalimbali.

Naye katibu mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Joseph Malongo alisema ukuta kama huo umejengwa Zanzibar na Tanga kwa zaidi ya Dola 5 milioni za Marekani. (Bakari Kiango)

Advertisement