Rais AfDB awakumbuka masikini kwa Sh1.15 bilioni

Muktasari:

  • Kutoa ni moyo, Waswahili walisema. Rais wa Benkiya Maendeleo Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina ametoa hela alizozawadiwa baada ya kushinda tuzo nchini Korea Kaskazini ili zisaidie kupambana na umasikini na kuwawezesha vijana kujiajiri.

Dar es Salaam. Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina ametoa Dola 500,000 (zaidi ya Sh1.15 bilioni) alizotunikiwa kwa kujitoa kwake zisaidie mapambano dhidi ya njaa, umasikini na ukosefu wa ajira Afri-ka.

Fedha hizo ni zawadi aliyoshinda baada ya kutunikiwa mshindi wa Sunhak Peace Prize mwaka 2019 aliyoshinda pamoja na Waris Dirie, mwanamke mwanaharakati anayepinga ukeketaji wa wananwake.

Tuzo za Sunhak hutolewa tangu mwaka 2015 kurithisha misingi ali-yokuwa akiiamina kiongozi maarufu wa kiroho nchini Korea Kas-kazini, Askofu Sun Moon.

Mshindi wa tuzo hizo zinazo-tolewa kila baada ya miaka miwili hupewa kitita cha Dola milioni moja (zaidi ya Sh2.3 bilioni) kuunga juhudi za kupambana migogoro, umasikini na uharibifu wa maz-ingira.

“Tunapambana kufungua fursa zilizopo Afrika.

Maisha yangu yatakuwa na maana endapo nita-fanikiwa kuwainua wengi kutoka kwenye lindi la ufukara,” amesema Dk Adesina anayefahamika kwa kujitoa kwake kupambana na uma-sikini duniani.

Akitangaza kutoa fedha zote alizopewa kwa kushinda tuzo hiyo mbele ya zaidi ya watu 1,000 walio-hudhuria sherehe hizo, Dk Adesina amesema lazima dunia iwajibike kumkomboa mtu masikini.

“Tunapaswa kupunguza tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasionacho. Kila mmoja anapaswa kuwa na kipato kukidhi mahitaji yake sio wachache peke yao. Leo hii masikini amekwama, anaku-la mabaki kama si makombo ya matajiri.

Kukosekana kwa usawa husababisha migogoro, sehe-mu yenye njaa haiwezi kuwa na amani” amesema Dk Adesina.

Amesema bila kujali rangi ya ngozi, kila taifa linapaswa kuhakik-isha wananchi wake wanakula vya kutosha ili waweze kuchangia shu-ghuli za maendeleo.Akiwa waziri wa kilimo wa Nigeria, Dk Adesina alishinda tuzo ya Jarida la Forbes mwaka 2013.

“Mpaka Juni, orodha ya mazao itakuwa inapatikana ili kuzisaidia kampuni za bima kuangalia mazao yapi waanze nayo na nimemwagiza kamishna wa bima kuharakisha mchakato wa uandaaji sera ili kuiwasilisha serikalini kwa hatua nyingine,” anasema Hasunga.