Standard Chartered yapata mkurugenzi mpya Mtanzania

Friday November 27 2015

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki ya Standard

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani. 

By Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Benki ya Standard Chartered Tanzania, imepata Mkurugenzi Mtendaji mpya ambaye ni Mtanzania, Sanjay Rughani.

Rughani amechukua nafasi ya Liz Lloyd ambaye amerudi makao makuu ya benki hiyo jijini London, Uingereza kuwa Mshauri wa Sheria wa benki hiyo.

Mkurugenzi huyo alijiunga na benki hiyo mwaka 1999 akiwa ni Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Fedha kisha alipanda cheo na kuwa meneja wa kitengo hicho barani Afrika, kazi ambayo aliifanya akiwa London.

Mkurugenzi wa benki hiyo Kenya na Afrika Mashariki, Lamin Manjang alisema anafurahi kumkaribisha tena Sanjay nyumbani Tanzania na pia katika timu yao ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Rughani alisema Tanzania ina fursa nyingi za biashara na kwamba, anafurahi kurudi nyumbani kuiongoza benki hiyo kwenda katika hatua nyingine ya maendeleo.

Alisema benki hiyo imejizatiti kutimiza malengo ya wateja.

Advertisement

Advertisement