WATANZANIA WAENDELEA KUISHUHUDIA TUZO YA KIMATAIFA YA KIZIBO CHA DHAHABU CHA TBL

Februari 28, 2020: Dar es Salaam: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeendelea kuionesha Tuzo ya kimataifa ya Kizibo Cha Dhahabu (IGCA) inayomaanisha Ubora wa Kimataifa kutokana na uzalishaji wa bidhaa zake bora kwa Watanzania ambapo hapo jana Tuzo hiyo iliwekwa Kituo cha Mabasi cha Morocco.  Tuzo hiyo ambayo kwa mara ya kwanza inakuja Afrika inakadiriwa kuwa na uzito wa kilo kilo 16.01 za dhahabu ambayo kwa bei za kimataifa ni sawa na Bilioni 2 za kitanzania. Miongoni mwa walioishuhudia tuzo hiyo ni Peter Mollel maarufu kwa jina la Pierre Liquid na mtanzaji Lil Ommy ambao kwa pamoja wameipongeza TBL kwa kutwa tuzo hiyo.

Leo siku ya Ijumaa tarehe 28 kizibo cha dhahabu kitaoneshwa makutano ya barabara ya Karume, Ilala kuanzia saa 5:00 kamili asubuhi hadi 8:00 mchana kisha kuelekea eneo la Buguruni, Ilala na kuoneshwa kuanzia saa 9:00 mchana hadi saa 12:00 kamili jioni.  Ziara ya maonesho ya kizibo itaishia siku ya Jumamosi, tarehe 29 katika maeneo mengine jijini Dar es Salaam.

Bidhaa zinazozalishwa na TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lite, Castle Lager, Castle Milk Stout, Redds Original, Budweiser, Balimi Extra Lager, Eagle Lager, Grand Malt na Safari Sparkling Water.

TBL group imeorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam, ikiwa na wafanyakazi takriban 1,700, inafanya uzalishaji katika mikoa minne ikiwa na vituo kadhaa vya usambazaji wa bidhaa zake.

-------------------------------------------------------------------

Kwa maswali au maelezo zaidi, wasiliana na:

Bi. Pamela Kikuli - Brand Manager; +255 767 266 415, [email protected]