Washindi wa droo ya tatu ya Mpawa wapatikana

Thursday June 27 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Benki ya CBA na Vodacom wametangaza washindi wa droo ya tatu leo kwa ajili ya promosheni yao ya kuadhimisha miaka mitano ya huduma ya Mpawa.

Promosheni hiyo imefanyika katika makao makuu benki ya CBA jijini Dar es salaam.

“Kampeni hii ya miaka mitano ya Mpawa imelenga kudumu kwa wiki 6 na leo ikiwa ni droo ya 3, tumekuwa na zaidi ya washindi 1,000 mpaka sasa tangu ilipoanza, ambapo baadhi ya washindi wameondoka na mara mbili ya akiba ya kuanzia na shilingi 1,000 mpaka 200,000, simu za kisasa, vocha pamoja na zawadi nyingine huku washindi wengine wakiongezeka kwenye droo zilizobaki,”amesema Maria Marbella ambaye ni mwakilishi wa benki ya CBA.

Amesema mshindi wa kwanza wa promosheni hiyo atazawadiwa Sh15 milioni kwenye droo ya mwisho hivyo amesisitiza watumiaji wa Mpawa kuweka akiba na kurejesha mikopo mapema ili waweze kupata nafasi ya kushinda.

Baadhi ya washindi wa droo ya Mpawa namba 1, 2 na 3 ni Mangu Zanura, Nyerenga Rahim, Robert Tuisenge na Mwafumba Martha.

Wengine ni Ayilla Agness, Kayombo Hilda, Mollel Charity, Gwandu Elizabeth, Agust Emannuel, Tezeyo Abinal na Mwita Joseph.

Advertisement

Washindi hao wametangazwa mbele ya mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu, Chiku Salehe.

 

Advertisement