Watu 157 wanahofiwa kupoteza maisha ajali ya ndege Ethiopia

Sunday March 10 2019

 

Addis Ababa, Ethiopia. Watu 157 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya ndege aina ya Boeing 737- 8 Max ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyokuwa ikielekea Nairobi kuanguka leo.

Kwa mujibu wa taarifa za ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia iliyotumwa kwa njia ya mtandao wa Twitter, ndege hiyo ilikuwa ikielekea Nairobi, Kenya.

Taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo zilifahamika dakika sita baada ya kuondoka kuelekea Nairobi, asubuhi ya leo saa mbili na robo na kuanza kupoteza mwelekeo ikiwa angani.

Ndege hiyo ilikuwa na abiria 149 na wafanyakazi wanane wa shirika la ndege nchini humo waliokuwa kwenye safari ya kuelekea Nairobi.

Advertisement