Papa Francis akataa watu waliooa kuwa mapadre

Thursday February 13 2020

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis 

Roma, Itali. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekataa pendekezo la kuruhusu watu waliooa kuwa mapadre.

Pedekezo hilo lilitolewa mwishoni mwa mwaka jana na maaskofu wa eneo la Amazon kwa kile walichodai kuwa ni kutokana na ukosefu wa watoa huduma hao.

Maaskofu hao pia walishauri wanawake kuwa wahudumu kanisani.

Kauli hiyo ya kiongozi huyo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa baada ya ile ya papa Benedikto 16 aliyekataa kuunga mkono hoja ya maaskofu hao wa Amazon.

Kupitia walaka wake wenye vipengee 111 chini ya kichwa cha habari Wapenzi Amazon, papa Francis alitoa wito wa wamisionari zaidi kutumwa katika eneo la Amazon na kuwahimiza maaskofu wote kutoka Marekani ya Kusini wajitolee zaidi katika kuwahimiza wale ambao wanataka kwenda likizo kwenda huko.

Advertisement