Uchaguzi unakuja na hofu Ivory Coast

Muktasari:

Idadi ya watu kati ya 3,000 waliopoteza maisha katika mapigano, wanatokeo eneo hilo, ambalo roho ya Ivory Coast katika uzalishaji wa cocoa na ni chanzo cha machafuko ya kikabila.

Duekoué, Ivory Coast (AFP). Kaka yake alikatwa koromeo na mpwa wake ambaye ni mlemavu, aliuawa kwa risasi nyumbani kwake, lakini Zeabahi Maurice ameweka pembeni mawazo ya kulipa kisasi kwa wanamgambo waliovamua kijijini kwao magharibi mwa Ivory Coast miaka kumi iliyopita.

Akiwa chifu wa Guitrozon, kijiji chenye watu karibu 1,400, Maurice anakumbuka matukio hayo vizuri.

“Jioni moja tulivamiwa na waasi kutoka kaskazini. Walianza kuua,” anasema.

Lakini wakati uchaguzi wa Oktoba 31 unakaribia, askari huyo wa zamani ambaye sasa ana miaka 75 anasema anafanya kazi bila kupumzika kusaidia kuzuia kujirudia kwa umwagaji damu katika Taifa hilo la magharibi mwa Afrika kama ilivyokuwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010-2011.

“Muhimu ni kutenda haki. Kila sehemu ambako mambo hayafanywi kwa haki, kuna vurugu. Tatizo la Ivory Coast kwa jumla ni ukosefu wa uaminifu,” anasema Maurice. “Lazima urudishwe (uaminifu).”

Idadi ya watu kati ya 3,000 waliopoteza maisha katika mapigano, wanatokeo eneo hilo, ambalo roho ya Ivory Coast katika uzalishaji wa cocoa na ni chanzo cha machafuko ya kikabila.

Vurugu ziliibuka baada ya Rais wa wakati huo, Laurent Gbagbo ambaye anatokeo magharibi, alipokataa kukubali kushindwa katika uchaguzi na Alassane Ouattara, Muislamu kutoka kaskazini.

Sasa, akiwa ameshaongoza kwa vipindi viwili, Ouattara anataka achaguliwe tena kuongoza kwa kipindi cha tatu kinyume na katiba iliyoweka ukomo, akisema mageuzi ya mwaka 2016 yalianzisha tena vipindi vya utawala.

Uamuzi wake ulikuwa chanzo cha maandamano, hasa katika mji ulio karibu wa Bangolo ambako maandamano yaligeuka kuwa vurugu, huku vijana wakichoma malori ya kampuni za madini ikiwa ni ishara kuwa rasilimali hazinufaishi wananchi.

“Hakuna shughuli za uzalishaji hapa,” alisema kwa hasira kiongozi wa vijana wa Bangolo, Gervais Gaha. “Ouattara hajafanya kitu. Tangu awe Rais watu wa kaskazini tu ndio wamenufaika.”

Utii umebadilika

Mzozo wa mwaka 2010-2011 uliambatana na mapigano baina ya watu wa kabila la Guere ambao ni wazawa wa eneo hilo, na wanaomuunga mkono Gbagbo, dhidi ya watu wa kabila la Dioula, kiasili wanatokea kaskazini na wengi wanamuunga mkono Ouattara.

Walioongezeka katika mchanganyiko huo ni wageni kutoka Burkina Faso, nchi jirani kwa upande wa kaskazini na ambayo watu wake wengi ni Waislamu, kama alivyo Ouattara.

Leo hii, tabia zao watu hao zinaendelea, lakini wamebadilisha utii.

Ouattara, 78, na rais wa zamani, Henri Konani Bedie, 86, na ambaye sasa ni kiongozi wa upinzani, wanasimama katika uchaguzi wa Oktoba 31.

Hata hivyo, Gbagbo, amezuiwa kugombea pamoja na Guillaume Soro, 48, waziri mkuu wa zamani na mshirika wa Ouattara ambaye alihamia upinzani.

Wakati wa mapigano, ambayo kila upande ulikuwa ukiutuhumu mwingine kuvamia, Soro aliongoza wanamgambo ambao walipambana na vikosi vya Gbagbo, ambaye sasa ana miaka 75.

Wanaharakati wa ardhi wako katikati ya masuala mengi yanayoibua chuki magharibi.

Mamadou Doumbia, kiongozi wa kidini mwenye ushawishi katika Jiji la Duekoue, alisema, “kampeni ya kuwazindua watu,” ambayo alishiriki, imesaidia kutuliza ushabiki, lakini alionya kuwa mizozo ya ardhi inaendelea ,“kujirudia” katika eneo “ambalo kila kitu kilianzia” katika vurugu za mwaka 2010.

Wazawa wa Gueres wanawatuhumu wageni kwa kuongeza ukubwa wa mashamba yao hadi katika ardhi waliyonunua au kukodi.

Kwa upande wa ndugu wa wageni, wahamiaji wa Dioulas na Burkinabe, pamoja na watu kutoka Baoule, wanawatuhumu Gueres kwa kutaka kuiba ardhi yao waliyonunua au kukodi kinyume cha sheria, mara baada ya kuboreshwa, “kwa jasho letu” kama mhamiaji mmoja kutoka Burkina Faso alivyosema.

Uchaguzi unaokuja unazidisha mgawanyiko kwa baadhi.

Marcellin Die, ambaye anaishi Duekoue na alikuwa kiongoza wa Chama cha Gbagbo eneo hilo, alisema: “Watu wa Gueres wanauawa kwa sababu ya imani yao. Duekoue ni mji wa watu hao. Tumechoshwa na mauaji yanayofanywa na chama cha RHDP (cha Ouattara).

“Sisi wananchi wa Ivory Coast tunataka nchi yetu!” alisema kwa nguvu. “Kazi iko kwa wafuasi wa Ouattara katika eneo lote.”

Katika Kjiji cha Maurice chenye watu karibu watu 1,400, wengi wao wakiwa Wagueres, kuna takribani kambi 50 za Wadioulas na Waburkinabes ambao wanafanya kazi katika mashamba ya cocoa.

Maurice bado anahofia mizozo midogo inaweza kuibuka.

“Watu wanasema, ‘tumechoshwa na watu hawa, hatuna budi kuwafukuza!” alisema Maurice.