Polisi washambulia wanywaji pombe Bujumbura; waua watatu

Saturday November 2 2019

Bujumbura, Burundi. Watu wenye silaha, waliovalia sare za polisi na jeshi wamewaua raia watatu mjini Bujumbura nchini Burundi. 

Shambulio hilo limefanywa katika baa moja katika Wilaya ya Rohero yenye ulinzi mkubwa na ambayo haina matukio mengi ya vurugu.

Aidha, katika tukio hilo, watu wengine watatu wamejeruhiwa.

Naibu msemaji wa polisi, Moise Nkurunziza alisema leo Jumamosi Novemba 2 kuwa, watu hao wasiofahamika walitumia silaha aina ya AK 47 waliwashambulia watu waliokuwa wameketi kwa amani wakipata vinywaji na kulipua guruneti.

Mmoja wa wanausalama waliopewa dhamana ya ulinzi kwenye eneo hilo alisema polisi wamefanya msako wa kuwatafuta wahusika mapema leo bila ya mafanikio yoyote.

Tukio hilo linajiri ikiwa ni miezi miwili tangu Umoja wa Mataifa (EU) uliposema kuwa Burundi inakabiliwa na hatari ya vurugu wakati ikielekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Advertisement


Advertisement