Afrika Kusini yathibitisha vifo viwili vilivyotokana na corona

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Zwelini Mkhize

Dar es Salaam. Wagonjwa wawili wa corona wamefariki dunia nchini Afrika Kusini huku maambukizi yakifika zaidi ya watu 1,000.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Zwelini Mkhize amesema kuwa kifo kimoja kimetokea katika hospitali binafsi na kifo kingine katika hospitali ya umma huko Western Cape.
Dk Mkhize ameongeza kuwa idadi kamili ya waliopatwa na ugonjwa huo itatolewa baadaye kidogo, lakini idadi ya wagonjwa imeongezeka hadi kufikia zaidi ya watu 1,000 tangu jana.
Vyombo vya ulinzi nchini humo, vimeanza kutekeleza agizo la kuzuia watu kutoka kwenye nyumba zao kwa wiki tatu, ili kupambana na virusi vya ugonjwa huo.
Katika zuio hilo, yeyote ambaye atakiuka agizo hilo atakabiliwa na kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini kubwa.