Aliyetoroka karantini kumfuata mpenzi afungwa jela

Muktasari:

Alitazamiwa kumaliza siku 14 za kujitenga juzi Jumatatu, lakini sasa atakaa mahabusu kwa mwezi mmoja baada ya kukiuka sheri za karantini

Mwananchi wa Australia ambaye amekuwa akitoroka karantini mara kwa mara na aliyeripotiwa kumtembelea mpenzi wake, leo amehukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela-- akiwa mtu wa kwanza kufungwa tangu nchi hiyo ipitishe sheria za kuzuia watu kutoka nyumbani ili kujinga na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.


Jonathan David, 35, alikamatwa mapema mwezi huu kutoka eneo la lazima la karantini katika hoteli ya jijini Perth, polisi wa Australia Magharibi walisema katika taarifa yao.


Aliiambia mahakama ya Perth kwamba kwanza alivunja sheria kwa lengo la kupata chakula lakini saa kadhaa baadaye akavunja tena sheria za karantini kwa sababu alimkumbuka mpenzi wake, shirika la habari la Seven News liliripoti.


BKwa kutoroka kupitia mlango wa dharura wa moto, aliwea kuwakwepa wafanyakazi wa hotelini lakini akaonekana katika kamera za usalama za CCTV, polisi walisema.


Chini ya sheria hizo zinazolenga kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona, David alitakiwa ajitenge kwa siku 14 baada ya kuwasili kutoka Jimbo la Victoria Machi 28.


Kama asingetoka hotelini kwake, angeachiowa huru Jumatatu lakini badala yake atatumia mwezi mzima jela na amelipishwa faini ya dola 1,280 za Kimarekani (sawa na takriban Sh2.2 milioni).


Polisi nchini Australia imeshalipisha faini zaidi ya 1,000 kwa makosa ya kukiuka sheria za kujifungia ndani, huku makosa yakiwa ni watu kukusanyika kushuhudia mashindano ya magari mitaani jijini Brisbane hadi kundi la watu waliokusanyika kula mkate wa nyama jijini Sydney.