Barnier aonya kupuuza athari za Brexit

Muktasari:

  • Waziri Mkuu wa Uingereza, Johnson Boris ameendelea kusisitiza nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), ifikapo Oktoba 31.

London, Uingereza. Mkuu wa mashauriano wa Umoja wa Ulaya (EU), Michel Barnier, ameonya dhidi ya kupuuza au kuchukulia kwa wepesi athari za nchi hiyo kujiondoa katika umoja huo bila ya makubaliano.

Barnier alisema masuala ambayo yameibuliwa na Uingereza ili kujitoa yanahitajika kujadiliwa kabla ya makubaliano kufikiwa.

Kiongozi huyo aliwaambia wabunge wa Umoja wa Ulaya kwamba makubaliano ya Brexit kuhusu haki za raia na mpaka wa Ireland, yatakuwa kama kiashirio cha mkataba wa baadaye kuhusu uchumi kati ya Uingereza na Umoja huo.

Aliongeza kuwa ikiwa Uingereza itajiondoa bila ya makubaliano, basi maswali yote yaliyoko kwa sasa hayatatoweka.

Barnier pia alisema kuwa miaka mitatu baada ya kura ya maoni iliyounga mkono Brexit, pande mbili hazipaswi kujifanya tu kwamba zinaendeleza mazungumzo.