Besigye; mwanasiasa aliyekamatwa na polisi mara nyingi duniani

Muktasari:

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda,  Kizza Besigye ametajwa katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kama kiongozi aliyekamatwa na polisi mara nyingi zaidi duniani.

Dar es Salaam. Kiongozi wa upinzani nchini Uganda,  Kizza Besigye ametajwa katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kama kiongozi aliyekamatwa na polisi mara nyingi zaidi duniani.

Katika taarifa ya kitabu hicho iliyotoka jana Jumanne Januari 20, 2020 imeeleza kuwa Besigye amekamatwa  mara 50 nchini Uganda, juzi Jumatatu ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa kiongozi huyo kukamatwa na polisi.

Rais huyo mstaafu wa chama cha Forum Democratic Change katika mara 50 alizokamatwa,  asilimia 30 ilikuwa mwaka 2016 ambako alikamatwa mara 15.