Bibi atumia saa nane kila siku kushona barakoa na kuzigawa bure

Bibi atumia saa nane kila siku kushona barakoa na kuzigawa bure
Hispania. Bibi mwenye umri wa miaka 84 hutumia masaa nane kila siku kwa ajili ya kushona barakoa (Mask) na kuzigawa kwa wafanyakazi wa afya kwa ajili ya kujikinga wakati wa kuhudumia wagonjwa wa corona


Margarita Gil Baro, kutoka Cadiz huko Hispania, ana uwezo wa kushona barakoa 50 kila siku kwa kutumia mashine yake ya kushona nyumbani na kuwapa wahudumu wa afya katika hospitali mbalimbali za nchi hiyo.
Bibi huyo hufanya hivyo kwa hiari kwa ajili ya kujitolea kuokoa maisha ya watu wakati huu ambapo dunia nzima inapambana na janga la kusambaa kwa virusi vya corona.


Katika picha aliyoweka katika mtandao wa Facebook Margarita anaonekana mwenye umakini na mvumilivu anaposhona vifaa hivyo muhimu kwa ajili ya kufunika mdomo na pua kuzuia virusi vya corona visiwaingie  binadamu.


Katika picha hiyo pia pembeni yake kuna rundo la barakoa ambazo tayari ametengeneza na huanza kazi hiyo saa nne asubuhi kila siku.
Mtoto wa bibi huyo aliiambia tovuti ya habari ya Hispania iitwayo Latina kwamba Margarita alimwambia:


"Siwezi kukaa bila kusaidia wakati hali hii ikitokea. Ninaelewa kuwa kila wakati kuna zaidi ambao wanaugua, na zaidi wanaokufa. Nitatengeneza vitambaa vya uso."


Margarita alisema wazo hilo lilimjia alipokuwa akitazama kwenye television jinsi hospitali nyingi zina uhapa wa barakoa za kuvaa usoni ndipo alipofikiria kama yupo nyumbani muda wote anaweza kusaidia kutengeneza


Uhaba wa barakoa za kuvaa usoni nchini Hispania umeripotiwa ambapo Serikali inategemea michango na watu wengi kujitolea kusaidia kutengeneza zao.