Boris Johnson apata ushindi mkubwa Uingereza

Muktasari:

Ushindi wa Conservative umesafisha njia kwa Borris kutimiza mpango wake wa kuiondoa Uingereza Umoja wa Ulaya (EU) baada ya miaka mingine ya kutokuwa na uhakika wa mustakabali wa nchi hiyo.

Waziri Mkuu Boris Johnson leo Ijumaa amesifu "tetemeko la kisiasa" baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi, ushindi ambao umesafisha njia kwa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya mwezi ujao baada ya miaka kadhaa ya mzozo wa kisiasa.
Huku karibu matokeo yote ya uchaguzi kwa ajili ya bunge lenye viti 650 yakiwa yameshatangazwa, chama cha Johnson cha Conservative kilikuwa kimeshashinda viti 362 -- ushindi wake mkubwa wa kwanza tangu enzi za Margaret Thatcher katika miaka ya themanini.
Lakini chama chas upinzani cha Labour kilikuwa na usiku mgumu, kikipoteza viti 59 na kushinda 203, kumlazimisha kiongozi wake Jeremy Corbyn kutangaza mipango ya kujiengua.
Chama kinachopinga kujiengua Umoja wa Ulaya cha Liberal Democrats kimesema kitambadili Jo Swinson kama kiongozi baada ya kushindwa kutetea kiti chake magharibi mwa Scotland ambako mgombea wa chama cha Scottish National Party (SNP) alishinda.
Fedha ya Kiingereza iliongezeka thamani jana Alhamisi jioni kw amatumaini kwamba Johnson sasa atatimizi ahadi yake ya kukamilisha kujiondoa Umoja wa Ulaya-- "Get Brexit Done"-- baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wa Uingereza.
Habari zaidi zinafuata