Boris aomba radhi Uingereza kuchelewa kujitoa EU

Sunday November 3 2019

 

Boris aomba radhi Uingereza kuchelewa kujitoa EU

London. Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amewaomba radhi Waingereza kwa kushindwa kuiondoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya (EU)  kufikia tarehe iliyopangwa Oktoba 31, mwaka huu.

Boris amesema “hali hii imenisikitisha sana, sana.”

“Ni suala la kujutia, Boris alikieleza kituo cha televisheni cha Sky News, kabla ya kumkosoa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kauli yake kwamba mpango wa Boris na EU utazuia biashara kati ya Marekani na Uingereza.

“Sitaki kumshambulia Rais lakini kwa mtanzamo huo bila shaka amekosea sana,” amesema.

“Kila mtu anayeutazama mpango wetu anaweza kuona jinsi ulivyo mzuri…unatupa nguvu zisizo na mipaka kusimamia viwango vyetu vya ushuru,” amesema.

Advertisement

Alhamisi iliyopita, Trump alimweleza rafiki yake Nigel Farage ambaye baadaye atakuwa mshindani wa Boris katika uchaguzi mkuu, kwa baadhi ya maeneo ya makubaliano hayo, huwezi kufanya biashara.

John alikuwa amesema bora afe mtaroni kuliko kuvumilia mchakato mrefu unaochosha wa kujitoa Brexit, ulioanza tangu mwaka 2016 kwa kura ya maoni iliyokuwa a ushindani mkali.

Leo ameelekeza lawama zote kwa Bunge la Uingereza kwa kushindwa kujitoa Oktoba 31 kwa kupitisha sheria ya kusogeza mbele.

Sheria hiyo iliitaka Serikali kuomba na kukubali kuongeza muda badala ya kujitoa kabla ya makubaliano hayajaridhiwa.

Wabunge walionyesha uungaji mkono wa awali, lakini wakivuta nyuma mpango wa Boris na kupitisha sheria hiyo kabla ya tarehe ya mwisho iliyokuwa imepangwa.

Suala la Uingereza kujitoa Ulaya limeendelea kuzua fukuto nchini humo huku likiwa tayari limesababisha mawaziri wakuu wawili, David Cameron na Theresa May kujiuzulu.

Advertisement