Corona yaua zaidi ya watu 100

Muktasari:

  1. Ujerumani imethibitisha mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo aliyepatikana katika mji wa mjini Munich.

Beijing, China.  Wizara ya Afya nchini China imesema kuwa watu 106 wamefariki dunia kutoka na ugonjwa wa corona.

Wizara hiyo ilisema kuwa mpaka leo asubuhi zaidi ya watu 4,000 wameripotiwa kuambukizwa virusi hivyo vilivyoanzia katika mji wa Wuhan, China.

Aidha, mgonjwa wa kwanza wa maradhi yanayosababishwa na virusi hivyo amethibitishwa nchini Ujerumani.

Msemaji wa Wizara ya Afya wa Ujerumani, alisema mgonjwa huyo mwanaume aliyetokea eneo la Stanberg, katika Jimbo la Bavaria lililopo kilomita 30 Kusini Magharibi mwa mji wa Munich.

Ndugu wa mgonjwa huyo walisema kuwa mwanaume huyo alianza kuwa na joto na mafua makali.

Virusi hivyo vipya vya aina ya Corona viliripotiwa kuanzia katika mji wa Wuhan nchini China mapema mwaka huu.

Tume ya Afya katika jimbo la Hubei ambako ni kitovu vya maradhi hayo imesema watu 24 wamekufa waliripotiwa kufariki jana na wengine 1,291 kuambukizwa idadi inayofanya jumla ya walioambukizwa hadi sasa kufikia 4,000.

Ugonjwa huo sasa umesambaa katika mataifa mbalimbali ikiwamo Korea Kusini, Taiwan, Thailand, Nepal, Vietnam, Saudi Arabia, Singapore, Marekani, Ufaransa, Australia, Singapore na Ujerumani.

Mlipuko wa ugonjwa huu umekuja wakati wa sherehe za mwaka mpya ambazo uwakutanisha mamilioni ya watu nchini humo wakisafiri kuwatembelea ndugu na marafiki zao.

Hata hivyo, mamlaka nchini humo imesogeza mbele kwa siku tatu mpaka Jumapili ijayo ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi

Marekani, ambayo ina maambukizi ya watu kadhaa, imewataka raia wake kufikiria upya suala la kusafiri kwenda China.