Dawa ya Chloroquine kutibu corona

Muktasari:

Wataalam wa afya nchini China wamesema dawa hiyo ya malaria imeonyesha ufanisi mzuri katika kutibu virusi hivyo.

Beijing, China. Dawa ya malaria aina ya chloroquine imedhibitisha kutibu virusi vya corona (covid-19)

Dawa hiyo iliyokuwa ikitumika zaidi kutibu ugonjwa wa malaria katika miaka ya 1980 na 1980 imeonyesha kutibu virusi hivyo baada ya kufanyiwa utafiti na wataalam wa afya wa nchi hiyo.

Wizara ya Afya sayansi na teknolojia ya   China, ilisema “chloroquine imethibitisha inaweza kutibu corona lakini pia ikakinga ugonjwa wa maralia kwa miongo kadhaa sasa.”

Shirika la habari la Xinhua limeripoti kuwa chloroquine imekuwa ikitumika kwa zaidi ya hospitali 10 ikiwamo moja iliyopo katika mji mkuu wa Beijing na mbili katika majimbo mengine.

Kwa mujibu wa Xinhua dawa hizo zimeonyesha ufanisi mzuri.