EU ‘yaitega’ Marekani kuhusu uamuzi wa kujiondoa mkataba wa Paris

Wednesday November 6 2019

Washington, Marekani. Umoja wa UIaya (EU) umesema kuwa imesikitishwa na kitendo cha Serikali ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya Paris yanayohusu mazingira.

Badala yake Umoja huo umesema una matumaini kuwa nchi hiyo ambayo ni moja ya watoaji wakubwa wa hewa inayochafua mazingira itabatilisha uamuzi wake na kujiunga tena.

Msemaji wa Halmashauri Kuu ya EU, Mina Andreeva alisema kuwa mkataba huo wa kimataifa uliotiwa saini mwaka wa 2015 unabaki kuwa makubaliano muhimu ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Msemaji huyo alisisitiza kuwa Umoja huo utaendelea kupambana na mabadilkiko ya tabia nchi chini ya mfumo huo wa kisheria licha ya kuondoka kwa Marekani.

Andreeva alisema Umoja huo utaendelea kufanya kazi na mashirika mbalimbali ya Marekani na wadau ambao wanadhamiria kuutekeleza mkataba huo.

Advertisement