Gavana Sonko apata dhamana

Muktasari:

Ni baada ya kusota rumande kwa siku tano.

Nairobi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Nairobi, imemuachia kwa dhamana gavana wa jiji hilo, Mike Sonko.

Hakimu mkazi mkuu, Douglas Ogoti alitoa uamuzi huo leo Jumatano Desemba 11 baada gavana huyo kukaa rumande kwa siku tano.

Gavana Sonko pamoja na maafisa wa Serikali walifikishwa mahakamani hapo Jumatatu iliyopita na kusomewa mashtaka ya ufisadi na kurudishwa rumande baada ya upande wa mashtaka kuweka pingamizi.

Awali Mkurugenzi wa mashataka ya umma Kenya, Noordin Haji aliagiza kukamatwa kwa gavana huyo kwa madai kuwa amehusika katika makosa ya ufisadi wa zabuni ya ujenzi.

Akitoa masharti ya dhamana hiyo, hakimu Ogoti alisema mtuhumiwa huyo anapaswa kuwa na bondi ya Sh30 milioni za Kenya karibu Sh690 za Tanzaniaa, kutoingia ofini kwake bila kibali au kusindikizwa na maofisa wa usalama.

Katika mashtaka hayo, Sonko na wenzake wanadaiwa kuhusika na upotevu wa fedha za umma Dola za Kimarekani 3.5 sawa na milioni 357 za Kenya

Gavana Sonko alikamatwa Ijumaa iliyopita katika mji wa Voi pwani ya Kenya muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa mashitaka ya umma nchini humo kusema kuwa ana ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka mwanasiasa huyo. Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alikana mashtaka hayo