Ghazouani ashinda urais Mauritania

Monday June 24 2019

 

Mauritania. Tume ya Uchaguzi nchini Mauritania, imemtangaza mgombea wa chama tawala cha Mauritania, Mohamed Ould Ghazouani kuwa mshindi wa nafasi ya uras wa nchi hiyo.

Ghazouani ambaye ni jenerali mstaafu wa jeshi na waziri wa zamani wa ulinzi,alitangazwa mshindi jana Jumapili June 24, baada ya kupata asilimia 52 ya kura zote zilizopigwa.

Mshindani mkuu wa Ghazouani ambaye ni mwanaharakati maarufu nchini humo anayepinga utumwa, Biram Dah Abeid ameshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 18 ya kura.

Mgombea mwingine, Sidi Ould Boubacar, anaeungwa mkono na chama kikubwa cha Kiislamu nchini humo alipata asilimia 17.87 ya kura.

Uchaguzi huo ni wa kwanza katika historia ya Taifa hilo lililopo katika jangwa la Sahara tangu lilipopata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960.

Advertisement