Huge Geingob ashinda urais Namibia

Muktasari:

Kiongozi huyo amepata asilimia 56.3 ya kura zote zilizopigwa na kumshinda mshindani wake, Panduleni Itula wa chama cha SWAPO.

Namibia. Rais Huge Geingob wa Namibia ameibuka kidedea baada ya kunyakua asilimia 56.3 ya kura zote zilizopigwa.

Tume ya Uchaguzi ya Namibia, imemtangaza Rais wa Namibia Geingob kuongoza katika kinyang’anyiro hicho na kumbwaga mpinzani wake, Panduleni Itula kutoka chama cha SWAPO aliyepata asilimia 29.4.

Rais huyo ametetea kiti chake ambako sasa ataogoza nchi hiyo katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.

Kiongozi wa chama cha upinzani, McHenry Venaani alishika nafasi ya tatu baada ya kupata asilimia 5.3.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo uliofanyika wiki iliyopita, Rais Geingob aliwashuruku Wanamibia wote kupitia kwa kumchagua tena kuwa Rais wao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter kiongozi huyo aliahidi kuboresha zaidi maisha ya raia wa nchi hiyo.

Hata hivyo, matokeo hayo yameonyesha kupungua kwa uungwaji mkono wa Rais Geingob baada ya kupungua kwa zaidi ya asilimia 30. Mwaka 2014 kiongozi huyo alichaguliwa kwa asilimia.

Awali wapinzani wa Rais huyo walidai uchaguzi huo ulikuwa na dosari kubwa ukilinganishwa na chaguzi nyingine.

Chama cha SWAPO kimeiongoza Namibia tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Afrika Kusini mwaka wa 1990.