Iran yazionya nchi za Magharibi; yadai itajibu mashambulizi

Tuesday November 26 2019

Iran. Jeshi la Iran limeionya Marekani pamoja na washirika wake wake kuacha kuchochea mgogoro uliopo katika nchi hiyo.

Wiki iliyopita wananchi wa Iran waliendesha maandamano wakishinikiza kushushwa kwa bei ya mafuta na kusababisha zaidi ya watu 100 kupoteza maisha. Bei ya mafuta ilipanda kwa asilimia 50.

Kupitia hotuba yake aliyoitoa leo Jumanne Novemba 26 kwa waandamanaji, kiongozi wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi cha jeshi la Iran, Jenerali Hossein Salami alisema Marekani iache kuchochea mgogoro huo kwa maslahi yake.

Jenerali Salami pia aliyatuhumu mataifa ya  Uingereza, Israel na Saudi Arabia kwa kuingia mgogoro huo.

Salami alitumia hotuba hiyo kuyaonya mataifa hayo ya Magharibi na kusema kuwa Iran itajibu kwa kuyaangamiza pindi yatakapo vuka mstari mwekundu. Hata hivyo, kiongozi huyo hakufafanua zaidi.

Hivi karibuni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International katika ripoti yake lilisema kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa wakati wa maandamano hayo.

Advertisement

Iran inaandamwa na uchumi unaosuasua tangu Marekani iliporejesha vikwazo baada ya kujtioa kutoka mkataba wa.

Advertisement