Italia yanasa 19 katika mtandao wa unga

Sunday November 3 2019

Rome. Polisi nchini Italia imewakamata watu 19 wengi kutoka Tanzania katika operesheni ya kuvunja mtandao wa usafirishaji dawa za kulevya.

Mtandao huo unajumuisha zaidi ya watuhumiwa 150 kutoka Afrika, Asia na Ulaya.

Kukamatwa kwa watu hao kunatokana na uchunguzi ulioanza tangu mwaka 2012 wakati polisi ilipokamata dawa za kulevya aina ya heroine kwenye mji wa Perugia katikati ya Italia.

Wachunguzi kwenye mji wa Peguria wamesema kiongozi mmoja wa mtandao huo ni Mtanzania aliyeishi Poland, ambaye aliagiza heroin kutoka Asia na kuingizwa Italia kwa ajili ya kuuza mitaani.

Mamlaka zimesema wasafirishaji wengi wa dawa za kulevya huficha utambulisho wao kwa kuishi kwenye makazi ya kawaida na kufanya kazi kama vinyozi, wachuuzi na katika taaluma nyingine rasmi.

Advertisement