Jinsi matangazo ya uongo ya video za matibabu yanavyoinuisha Youtube

Monday September 16 2019

 

London, Uingereza. Uchunguzi uliofanywa na BBC, umebaini kuwa kuna video za lugha mbalimbali katika chaneli za Youtube, zinazotoa taarifa ambazo sio sahihi za matibabu ya saratani.

Kwa mujibu wa BBC, matangazo yanayoongoza kwa taarifa za uongo ni video za bidhaa mbalimbali na vyuo vikuu.

Uchunguzi huo umebaini kuwa kuna video zaidi ya 80 zinazotumia lugha tofauti za aina 10 zinarushwa katika mtandao wa Youtube.

“BBC ilibaini zaidi ya video 80 ambazo zina maudhui ya afya ambayo sio sahihi haswa ya ugongwa wa saratani,” lilisisitiza shirika hilo.

Shirika hilo lilienda mbali zaidi na kusema kuwa katika video 10 zilizochunguzwa tayari watu zaidi ya milioni waliangalia.

Advertisement