Johnson shinda kwa kishindo Uingereza

Muktasari:

Waziri huyo mkuu amesema baada ya ushindi huo mkubwa atahakikisha anakamilisha mpango wa kujiondoa Umoja wa Ulaya (EU) mapema kabla ya siku ya mwisho ya Januari 31 mwakani ili kutimiza utashi wa Waingereza.

Waziri Mkuu Boris Johnson leo Ijumaa amesema atahakikisha utashi wa Waingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya unatimizwa baada ya chama chake kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi.
Ushindi huo umesafisha njia kwa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya mwezi ujao baada ya takriban miaka mitatu ya kusuasua.
Kwa maana hiyo, Uingereza itajiondoa Umoja wa Ulaya Januari 31 mwakani kama ilivyopangwa.
Akishutumu kipindi cha zaidi ya miaka mitatu ya mzozo wa kujiondoa Umoja wa Ulaya, maarufu kwa jina la Brexit, Johnson alisema: "Nitamaliza vitu vyote vya kipuuzi na tutatimiza mpango wa Brexit ndani ya muda, yaani Januari 31, hakuna cha hapa, hakuna cha lakini."
Huku karibu matokeo yote ya uchaguzi kwa ajili ya bunge lenye viti 650 yakiwa yameshatangazwa, chama cha Johnson cha Conservative kilikuwa kimeshashinda viti 362 -- ushindi mkubwa wa kwanza wa chama hicho tangu enzi za Margaret Thatcher katika miaka ya themanini.
Lakini chama chas upinzani cha Labour kilikuwa na usiku mgumu, kikipoteza viti 59 na kushinda 203, kumlazimisha kiongozi wake Jeremy Corbyn kutangaza mipango ya kujiengua.
Chama kinachopinga kujiengua Umoja wa Ulaya cha Liberal Democrats kimesema kitambadili Jo Swinson kama kiongozi baada ya kushindwa kutetea kiti chake magharibi mwa Scotland ambako mgombea wa chama cha Scottish National Party (SNP) alishinda.
Fedha ya Kiingereza iliongezeka thamani jana Alhamisi jioni kwa matumaini kwamba Johnson sasa atatimizi ahadi yake ya kukamilisha kujiondoa Umoja wa Ulaya-- "Get Brexit Done"-- baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wa Uingereza.
Akiwa na wabunge wengi. Johnson ataweza kufanikisha mpango wa kujiondoa ambao alikubaliana na Umoja wa Ulaya kwa kupitia Bunge kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Januari 31.
Kusaini mpango huo kutamaliza miongo takriban mitano wa undudu wa Uingereza na Umoja wa Ulaya, ingawa pande zote bado zinahitaji kufanyia kazi masuala ya biashara na usalama.
Waziri wa Mambo ya Ulaya wa Ufaransa. Amelie de Montchalin alikuwa mwanasiasa wa kwanza kukubaliana na "ushindi wa dhahiri mkubwa, kitu ambacho kilikuwa kinakosekana nchini Uingereza kwa miaka kadhaa".
Unaashiria ushindi binafsi wa Johnson, meya wa zamani wa London na waziri wa mambo ya nje ambaye aliongoza kwa mafanikio kampeni ya kujiondoa Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni iliyofanyika mwaka 2016.
rais wa Marekani, Donald Trump aliandika katika akaunti yake ya Twitter akiuzungumzia ushindi huo kuwa ni mkubwa na kusema kwamba Marekani na Uingereza zitaweza kuingia mikataba mingi mipya ya kibiashara baada ya Brexit.
"Mpango huo una uwezekano wa kuwa mkubwa zaidi na wenye fedha kuliko mingine yoyote ile ambayo ingeweza kufanywa na Umoja wa Ulaya. Mshangilie Boris!" alisema.

Taking the north -
Chama cha Conservatives kimekuwa kikiongoza katika kura za maoni kwa wiki kadhaa lakini kiwango cha ushindi hakikutarajiwa.
Chama hicho kilichukua viti ambavyo kw akawaida huchukuliwa na Labour na ambavyo havijawahi kwenda kwa chama cha Johnson kwa miongo kadhaa, lakini vingi vikiwa viliunga mkono mpango wa kujiondoa Ulaya wa mwaka 2016.
"Sasa hatuna budi kuelewa ni tetemeko la aina gani tulilitengeneza," alisema Johnson alipoongea na wafanyakazi wa chama chake, kwa mujibu wa shirika la habari la Press Association.
Awali alitangaza baada ya kuchaguliwa tena kuwa mbunge kuwa wapigakura wamempa "nguvu kubwa mpya ya kufanikisha Brexit".
Johnson sasa ataongoza kwa miaka mitano kabla ya kulazimika kuitisha uchaguzi mwingine.

Labour yaanguka -
Kwa kulinganisha Labour ilikuwa ikielekea katika kipigo chake kikubwa tangu mwaka 1935, kikiwa na viti 203, baada ya Corbyn kukiri kwamba ulikuwa ni "usiku mbaya sana".
Alisema atang'atuka baada ya kipindi cha kutafakari na hatakiongoza chama hicho katika uchaguzi ujao, ambao utafanyika 2024.
Corbyn alikuwa ameahidi kuitisha kura ya pili ya maoni kuhusu kujiondoa Ulaya, ikiwa ni jitihada za kuvutia nusu ya wapigakura wa Uingereza ambao bado wanataka kuendelea kuwa ndani ya Umoja wa Ulaya.
Lakini kampeni zake za Labour zilijikita zaidi katika mabadiliko ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kutaifisha tena viwanda muhimu, lakini hakuweza kuvutia wapigakura.
Akizungumza mapema leo Ijumaa, Corbyn alitetea ilani ya chama chake mna kusisitiza kuwa sera yake zilipendwa na wengi wakati wa kampeni.
Lakini alisema: "Brexit ilifunika na kugawanya watu wa nchi hii, ilifunika sana masuala ya mijadala ya kawaida ya kisiasa."