Kesi ya waziri mkuu Israel yaiva

Muktasari:

Waziri mkuu, Benjamin Netanyau anakabiliwa tuhuma za rushwa, kughushi na kuvunja uaminifu ambako. Kesi hiyo sasa kuanza kusikilizwa Machi 17.

Yerusalemu, Israel.  Kesi ya ubadhirifu inayomsubiri Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau itaanza kusikilizwa rasmi Machi 17.

Taarifa ya wizara ya sheria ya nchi hiyo ilisema katika kesi hiyo Netanyahu atasomewa mashitaka dhidi yake yatakayosomwa na jopo la majaji watatu.

Mashtaka hayo ni pamoja na kupokea rushwa, kughushi na kuvunja uaminifu.

Netanyahu ambaye ni waziri mkuu wa kwanza wa Israel kushtakiwa akiwa madarakani amenukuliwa mara kwa mara akisema tuhuma dhidi yake ni za uongo zeye lengo la kumchafua kisiasa.

Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa  kiongozi huyo anatarajiwa kukiongoza chama chake cha Likud katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 2.

Uchaguzi huo umekuja kufuatia ule wa Aprili na Septemba mwaka jana kukosa mshindi.

Israel inaingia katika uchaguzi wa tatu wa kitaifa katika muda wa mwaka mmoja.