Kiongozi wa upinzani Cambodia aachiwa huru

Muktasari:

Ni Kem Sokha, aliyekuwa akitumikia kifungo cha kukaa nyumbani kwa zaidi ya miaka miwili kwa kosa la  uhaini.

Combodia, Colombia. Mahakama ya Cambodia imemuachilia huru kiongozi wa upinzani aliyekuwa akitumikia kifungo cha kukaa nyumbani kwa zaidi ya miaka miwili.

Kem Sokha, kongozi wa upinzani nchini humo alikuwa akishtakiwa kwa kosa la uhaini.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Sokha alikamatwa mwaka 2017 na kutuhumiwa kupanga njama za kuipindua Serikali ya Waziri Mkuu, Hun Sen ambaye ametawala tangu 1985.

Sokha ni mwanzilishi mwenza wa chama cha upinzani cha National Rescue ambacho kilifutwa kabla ya uchaguzi uliompa ushindi Hun Sen mwaka jana.

Uamuzi mpya wa mahakama ambao ulitaja sababu za kiafya, unamkataza kiongozi huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 66 kusafiri nje ya Cambodia au kujiunga na shughuli za kisiasa.