Maandamano Ufaransa yamchomoa Rais Macron

Monday December 9 2019

Ufaransa. Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ameitisha baraza la mawaziri ili kujadili mgogoro uliopo baina ya wafanyakazi wa umma na Serikali.

Kwa siku nne mfululizo wafanyakazi wa umma nchini humo wameendesha maandamano kupinga fomula mpya ya mafao ya jamii.

Rais Macron, Waziri Mkuu, Edouard Philippe pamoja na mawaziri wengine katika baraza hilo wamekutana jana Jumapili kujadili mabadiliko hayo katika malipo ya uzeeni yaliyotangazwa mwanzoni mwa wiki hii.

Hata hivyo, siku moja baada ya Serikali ya Rais Macron kutangaza mabadiliko hayo, wananchi wa Ufaransa walishiriki maandamano makubwa  na kusababisha huduma za msingi kusimama ikiwamo usafiri wa umma baada ya treni kuacha kufanya kazi.

Maandamano hayo yaliyoanza Alhamisi iliyopita yameratibiwa na vyama vya wafanyakazi.

Katika madai hayo, waandamanaji hao kutoka makundi ya kada mbalimbali wanadai mabadiliko hayo yatasababisha kufanya kazi kwa muda mrefu na kupata malipo kidogo pindi wanapostaafu.

Advertisement

Inaelezwa kuwa zaidi ya watu laki nne waliandamana katika siku ya kwanza ya maandamano hayo yaliyokuja kipindi ambacho uchumi wa Ufaransa umeanza kutetereka.

Advertisement