Makamu wa Rais Iran akutwa na maambukizi ya virusi vya corona

Makamu wa Rais Iran anayeshughulikia wanawake na masuala ya familia, Masoumeh Ebtekar

Iran. Makamu wa Rais Iran anayeshughulikia wanawake na masuala ya familia, Masoumeh Ebtekar na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Usalama na Mambo ya Nje, Mojtaba Zolnour wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Iran imeeleza Ebtekar amekuwa kiongozi wa kwanza katika baraza la Rais, Hassan Rouahni kupata maambukizi hayo.

Zolnour alijitangaza kupitia video akisema amepata maambukizi ya ugonjwa huo ambao ushaua watu zaidi ya 2,700 duniani huku China ikiwa ni mwathirika zaidi.

Mbali ya hao tayari Naibu Waziri wa Afya, Iraj Harirchi alijirekodi video akieleza maambukizi ya ugonjwa huo na kuwapa matumaini wananchi.

Hadi sasa Iran humo waliokufa ni 26 na 245 wameambukizwa