Mambo magumu kwa waziri Netanyau

Muktasari:

  • Akabiliwa na ushindani mkali katika Uchaguzi Mkuu wa nafasi ya uwaziri mkuu wan chi hiyo.

Israel. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ambaye anawania nafasi hiyo kwa muhula wa nne mfululizo anakabiliwa na ushindani mkali.
Wananchi nchini Israel wameanza kupiga kura jana katika uchaguzi utakaoamua iwapo Waziri Mkuu wa sasa ataendelea kuwemo madarakani huku akiwa katika wasiwasi wa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuhusika na ufisadi.
Waziri Mkuu huyo ambaye amekuwamo madarakani kwa muda mrefu zaidi kuliko mwengine yeyote anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa jenerali mstaafu Benny Gantz. Chama cha jenerali huyo mstaafu cha Buluu na Nyeupe kiko sambamba na chama  cha Netanyahu cha Likud.  Hata hivyo vyama hivyo vitalazimika kuunda mseto na vyama  vidogo itakapobidi kuunda serikali. Leo asubuhi Rais wa Israel Reuven Rivlin alipiga kura katika mji wa Jerusalem na alisema kuwa leo ni israel inasherehekea demokrasia.
Waziri Mkuu Netanyahau amejaribu kujinadi kuwa yeye ni kiongozi mwenye sifa za kipekee za kuiongoza  nchi katika nyakati za changamoto lakini mshindani wake anamzungumzia  Netanyahu kuwa Waziri Mkuu anayeigawanya nchi na pia mwanasiasa anayeandamwa na kashfa.
Katika uchaguzi hil Gantz anajinadi kama mtu mtulivu na mwadilifu.
Akizungumza wakati wa kupiga kura, Gantz alisema Waisraeli wanapiga kura ya mabadiliko.
Kiongozi huyo wa chama cha Bluu na Nyeupe, alisema chama chake kitafanikiwa kuleta matumaini, bila rushwa na kuwapo misimamo mikali.