Mawaziri watano watangaza kujiuzulu Uingereza

Wednesday October 9 2019

London, Ungereza. Kundi la mawaziri watano liko mbioni kujiuzulu kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutofatiana na mpango wa Waziri Mkuu, Borisi Johnson.

Waziri mkuu Boris anakabiliwa na upinzani mpya kutoka kwa baraza lake la mawaziri kutokana na wasiwasi wa kutofikiwa kwa makubaliano ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya (EU) maarufu kama Brexit.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo Jumatano Oktoba 9, katika gazeti la The Times, kundi la mawaziri hao limepanga kujiuzulu ili kupisha mpango huo.

Gazeti hilo liliwataja mawaziri walio katika orodha hiyo kuwa ni pamoja na Nicky Morgan (utamaduni), Julian Smith (anayehusika na Ireland Kaskazini), Robert Buckland (sheria), Matt Hancock (afya) na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo, Geoffrey Cox.

Gazeti hilo lilimnukuu mmoja wa mawaziri hao ambaye hata hivyo, hakutaka kutajwa jina lake akisema kuwa idadi kubwa ya wanachama wa Conservative watajiuzulu iwapo hakutakuwa na makubaliano ya Brexit.

Advertisement