Mbunge achomwa kisu

Wednesday November 6 2019

 

Beijing, China. Mmoja wa waandamanaji anayeipinga Serikali, amemchoma kisu na kumjeruhi mbunge wa Hong Kong.

Mbunge huyo anayeiunga mkono serikali ya Beijing, alikuwa akifanya kampeni ya uchaguzi hii leo.

Tukio hilo la karibuni linaashiria kuongezeka kwa machafuko yanayohusiana na maandamano ya kudai mageuzi ya kisiasa katika jimbo hilo la China lenye mamlaka ya ndani.

Mbunge Junius Ho amekuwa kiongozi anayechukiwa na waandamanaji kutokana uhusiano wake na serikali na matumizi ya nguvu dhidi yao.

Taarifa ya Serikali kwa vyombo vya habari, imelaani shambulizi hilo na polisi imesema imemkamata muandamanaji aliyefanya tukio hilo.

Advertisement