Mgonjwa wa corona agundulika Kenya

Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe

Dar es Salaam. Serikali ya Kenya imethibitisha kuwapo kwa mgonjwa wa  kwanza  aliyekutwa na virusi vya corona abaye ni mwanamke aliyeingia nchini humo akitokea Marekani na kupitia London Uingereza.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe akizungumza leo Ijumaa, Machi 13, 2020 ameeleza kuwa licha ya kuwa mgonjwa huyo kuwa na hali nzuri ya kuweza kula chakula bado hataruhusiwa kutoka hospitalini hadi pale atakapopimwa tena na kukutwa hana virusi hivyo.
Mwanamke huyo amewekwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta katika kitengo cha magonjwa ya kuambukiza.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeshafatilia na kubaini kote alipopita mwanamke huyo na watu aliokutana nao tangu alipowasili nchini humo.
Wakati huo huo Kenya imesitisha safari zote za nje ya nchi isipokuwa zile zenye ulazima.